Mwenyekiti wa makundi mbalimabali ya jamii ya watu wanaoishi na uwezo maalum katika ukanda wa Pwani Bi. Hamisa Maalim Zaja, ameitaka jamii kuacha itikadi za kale za kuwashirikisha walemavu wa ngozi na mambo ya ushirikiano.
Bi. Zaja anasema ni wakati sasa kwa jamii kuwatazama watu wenye ulemavu wa ngozi kama watu wengine katika jamii na kuwapa nafasi ya kutambulika badala ya kuwaweka katika maisha ya wasiwasi.
Bi. Zaja amesema jamii inafaa kuweka kando itikadi za kale kwani walemavu wa ngozi wanahaki kama wananchi mwengine wa kawaida.
Taarifa Na Hussein Mdune