Watangazaji wa Radio Kaya walijumuika na Jamii ya mbalimbali za Wamijikenda katika kituo cha utamaduni cha Rabai Cultural village katika maeneo ya Rabai kaunti ya kusherehekea mwaka mpya wa Jamii ya Warabai.
Sherehe hizo za kitamaduni zilijumuisha ngoma mbalimbali za kitamaduni, vyakula asilia, mavazi ya kitamduni miongoni mwa vitu vingineo huku jamii hiyo ikizihimiza jamii mbalimbali za Wamijikenda kuendelea kuuenzi utamaduni wao.
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Kaya Rabai Mzee Daniel Garero amewahimiza vijana kuenzi utamaduni wao badala ya kutekwa na mila za kimagharibi kwani hatua hiyo itachangia zaidi uendelezaji wa utamaduni wa jamii ya Wamijikenda kanda ya pwani.
Kwa wake Mkurugenzi wa idara ya utamaduni, maswala ya kijamii na michezo katika kaunti ya Kilifi, ,,, amewahimiza wapwani hasa wanatokea jamii ya wamijikenda kushirikiana na serikali ya kaunti hiyo katika kufanikisha maswala ya utamaduni ili kuinua uchumi wa Pwani.