Jamii ya watu wanaoishi na ulemavu imehimizwa kujiandikisha na baraza la kitaifa la watu wanaoishi na ulemavu ili kupewa kadi maalum ya utambulisho.
Mwenyekiti wa kamati ya hazina ya kitaifa ya watu wanaoishi na ulemavu Profesa Julia Ojiambo amesema kuwa kadi hizo zina umuhimu mkubwa kwa kila mtu anayeishi na uwezo maalum.
Ojiambo aidha ametaja kuwa kadi hizo zinawasaidia watu wanaoishi na uwezo maalum kupata misaada mbalimbali kutoka kwa serikali na mashirika ya yasiokuwa ya kiserikali.
Kauli yake inajiri huku shirika la kitaifa linaloshughulika na wanaoishi na uwezo maalum likiendelea kugawa vifaa mbali mbali kwa walemavu ukanda wa Pwani kujiendeleza.
Taarifa na Mariam Gao.