Story by Gabriel Mwaganjoni-
Jamii ya walemavu katika kaunti ya Mombasa imelalamikia kupitia hali ngumu ya maisha pindi watu hao wanapozuru hospitalini ili kutafuta huduma za kiafya.
Wakiongozwa na Florence Hare, aliye mlemavu wa macho, amesema watu hao wanaokumbwa na changamoto za kimaumbile wamekuwa wakipitia changamoto hospitalini hasa za umma kwani hazina wataalam wa afya wanaofahamu lugha ya ishara.
Akizungumza katika kaunti ya Mombasa, Hare vile vile amefichua kwamba watu hao wamekuwa wakihangaishwa na maafisa wa polisi kwani wengine hasa walio na ulemavu wa kusikia hutazamwa na maafisa hao kama wajeuri.
Mwanaharakati huyo kwa sasa anataka haki za jamii hiyo ya walemavu kuzingatiwa kikatiba.