Picha kwa hisani –
Viongozi wa jamii za wafugaji kutoka maeneo mbali mbali ya nchini wamefanya kikao na kinara wa ODM Raila Odinga jijini Nairobi ili kueleza msimamo wao kuhusu ripoti ya BBI.
Wakiongozwa na mbunge wa Eldas Adan Keynan viongozi hao wamesema wanaunga mkono mchakato wa kufanyia marekebisho katika ya nchini wa BBI kwani baadhi ya mapendekezo yao yamejumuishwa kwenye ripoti hio.
Kwa upande wake waziri wa fedha nchini Ukur Yattani aliye mmoja wa viongozi wa wafugaji, ametoa hakikisho kwa kiongozi wa nchi Uhuru Kenyatta na Odinga kwamba jamii ya wafugaji haitobadili msimamo wao kuhusu ripoti hio ya BBI.
Naye Kinara wa ODM Raila Odinga amesema watahakikisha jamii ya wafugaji haiachwi nje kwenye mazungumzo kuhusu ripoti ya BBI ili kuhakikisha mapendekezo yote ya jamii hio yanajumusihwa katika ripoti hio.
Viongozi hao wa jamii ya wafugaji waliohudhuria mkao huo ni pamoja na magavana, mawaziri,makatibu ,wabunge na spika wa mabunge ya kaunti mbali mbali nchini.