Story by Our Correspondents
Mgombea wa kiti cha uwakilishi wadi ya Puma katika eneo bunge la Kinango kaunti ya Kwale kwa tiketi ya chama cha Wiper, Mrinzi Nyundo Mrinzi amewataka wakaazi wa Puma kuthamini baadhi mila na tamaduni zao.
Mrinzi amewasifu wakaazi wa kijiji cha Fingoni katika eneo la Vigurungani kwa kuhifadhi sehemu ya taambiko ,akisema eneo hilo ni muhimu kwa wazee kufanya tambiko dhidi ya matatizo wanayopitia wanajamii.
Mrinzi amezisihi jamii zinazoishi katika wadi hiyo ya Puma kubadilisha mkondo wao wa maisha kwa kuzihifadhi sehemu nyenginezo zinazoaminika kuwa takatifu, akitaja mabadiliko ya anga kama yanayochangiwa na jamii kusahamu tamaduni zao.