Picha kwa hisani –
Baadhi ya wakereketwa wanaoangazia masuala ya mtoto wa kike nchini wameishauri jamii katika Kaunti ya Kwale kutowahurumia watu wanaochangia watoto wa shule kupata mimba za utotoni.
Kulingana na afisa mkuu wa shirika la Ahadi Kenya Stanely Kamau ni kuwa huenda watoto wengi wakakosa kurudi shule mwakani kufuatia kupata ujauzito .
Wakati uo huo Kamau amewaomba wazazi kuwalinda watoto wao huku akiitaka jamii kutokubali kusuluhisha visa vya dhulma za watoto nyumbani .
Aidha Stanely amesema kulingana na repoti waliyopokea katika shirika lao ni kuwa idadi ya watoto wanaohofiwa kupata ujauzito kwenye Kaunti hiyo huenda imepanda wakati huu ambapo wapo nyumbani.