Story by Mwahoka Mtsumi –
Jamii kaunti ya Kwale imehimizwa kukumbatia mpango wa upanzi wa miti katika maeneo ya makaazi ili kuhifadhi mazingira.
Mwenyekiti wa walimu wa mazingira kaunti ya Kwale Hassan Mwadima amesisitiza haja ya jamii kupanda miti, akisema hali hiyo itachangia kushuhudiwa kwa mvua kwa wingi na kuchangia mazao mengi shambani.
Kwa upande wake Msimamizi wa masuala ya usalama na Mazingira katika kampuni ya Base Titanium Geofrey Mwanya ameirai jamii kuwa mstari wa mbele katika kuhifadhi mazingira.