Story by Mwahoka Mtsumi –
Naibu Jaji mkuu nchini Bi Philomena Mwilu amewahimiza wakenya kuhakikisha kesi wanazowasilisha Mahakamani zina ushahidi wa kutosha ili kuzuia mkanganyo wa kusikizwa kwa kesi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mkakati maalum wa Tume ya uiano na utangamano wa kitaifa NCIC, Jaji Mwilu amesema ushahidi wa kutosha utachangia mahakimu kutoa uamuzi wa haki.
Jaji Mwili amesisitiza haja ya ushirikiano wa idara zote za kiserikali nchini ambazo zinahusika pakubwa katika kuwasilisha kesi zinazohusu haki ya wananchi ili kuhakikisha haki ya mkenya inapatikana.
Kwa upande wake Waziri wa usalama wa ndani Dkt Fred Matiang’i amesema serikali imeweka mikakati muafaka ya kuhakikisha kila mkenya anakuwa na usalama wa kutosha wakati huu ambao taifa linapoelekea katika uchaguzi mkuu.