Picha kwa hisani –
Jaji mkuu nchini David Maraga amewataka wakenya kuhakikisha wanapinga vikali marekebisho ya katiba kupitia mchakato wa BBI ambayo yanalenga kuikandamiza idara huru ya Mahakama nchini.
Akizungumza katika majengo ya Mahakama ya upeo kule Nairobi wakati wa halfa ya kutoa ripoti ya utendakazi wa idara ya Mahakama ya mwaka wa 2019/2020, Jaji Maraga amesema idara ya Mahakama inafanya kazi vyema na inaifai kuhujumiwa.
Maraga amesema japo anastaafu mapema mwakani, ana furaha kufanikisha ndoto za idara ya Mahamana nchini licha ya maswala mengi muhimu kukosa kuafikiwa huku akisema hana tofauti za binafsi kati yake na Rais Uhuru Kenyatta.
Wakati uo huo amesema kati ya mwezi Januari mwaka 2017 hadi mwezi Juni mwaka huu, Idara ya Mahakama wamefanikiwa kusuluhisha kesi laki 2, elfu 1,206 zilizosalia Mahakamani kwa zaidi ya miaka 5.