Picha kwa Hisani –
Jaji Martha Koome ameapishwa rasmi kuwa Jaji mkuu wa kwanza mwanamke nchini baada ya jina lake kuchapishwa katika gazeti rasmi la Serikali na Rais Uhuru Kenyatta.
Halfa hiyo ya kuapishwa kwa Jaji Koome imefanyika katika Ikulu ya Nairobi na kuongozwa na Msajili mkuu wa idara ya Mahakama nchini Anne Amadi ikishuhudiwa na Rais Uhuru Kenyatta.
Akichukua kiapo cha kuisimamia idara ya Mahakama nchini kama Jaji mkuu na Rais wa Mahakama ya Upeo, Jaji mkuu nchini Martha Koome aahidi kuzingatia katiba ya nchi, kuwa muadilifu, kuwajibikia kikamilifu shuhuli za idara ya Mahakama bila ya kushurutishwa na mtu yeyote.
Baada ya kuapishwa kwa Jaji mkuu nchini Martha Koome, Jaji William Ouko pia amekula kiapo cha kuhudumu kama Jaji wa Mahakama ya Upeo nchini huku akiahidi kuwajibikia majukumu yake vyema kwa kuzingatia haki na usawa.
Hata hivyo Rais Kenyatta aliyeshuhudia kuapishwa kwa majaji hao amewahimiza majaji nchini kuzingatia haki na usawa katika majukumu yao ya kikazi, kujitenga na msukumo wa kisiasa, kuheshimu idara ya Mahakama, na kutoogopa lolote.