Picha Kwa Hisani.
Mwanamuziki wa reggae Siccature Alcock almaarufu Jah Cure atahudumu kifungo cha miaka sita gerezani kwa jaribio la kuua bila maksudi.
Mzaliwa huyo wa Jamaica alihukumiwa kifungo hicho na mahakama moja nchini Uholanzi siku ya Jumanne.
Picha Kwa Hisani.
Mnamo mwezi Oktoba mwaka jana, Jah Cure, 43, alishtakiwa kwa kosa la kumdunga kisu promota Nicardo ‘Papa’ Blake.
Mzozo wao ulihusisha takriban shilingi 630, 000 ambazo Jah Cure alimdai promota huyo kama malipo ya tamasha alilokuwa amefanya mjini Dam Square, Uholanzi. Jah Cure alikuwa anatazama kifungo cha hadi miaka 15 gerezani.
Picha Kwa Hisani.
Akijitetea mahakamani mapema mwezi huu, mwanamuziki huyo alisema alikuwa anajikinga ila mahakama ikakataa madai yake. Upande wa mashtaka ulisema alikusudia kumsababisha Blake majeraha mwilini.
Mahakama hata hivyo haikumpata na hatia ya jaribio la mauaji na badala yake akatiwa hatiani ya kujaribu kuua bila kukusudia.
Picha Kwa Hisani.
Jah Cure aliwahi kuhudumu kifungo kingine cha miaka 8 kati ya 1999-2007. Alikuwa amepatikana na makosa ya wizi wa kimabavu, umiliki haramu wa bunduki na ubakaji.