Picha kwa hisani –
Muigizaji wa sinema za Bongo, Jackline Wolper ameibuka na jipya na kusema
kuwa mwanaume atakayeweza kumpa ujauzito, atamkirimia kwa kumjengea
nyumba ya kisasa yenye mahitaji muhimu ya kibinadamu.
Akizungumza kupitia kituo kimoja cha habari mjini Dar Es Salaam, muigizaji
huyo ameahidi kumzawadia mwanamume yeyote atakaye mpa mtoto wa jinsia
yoyote ile. Hii ni baada ya mashabiki wake kumuuliza kuhusu kujipanga kwake na
swala la malezi.
“…Kila nikikatiza maneno ni hayo hayo. Sasa mimi nasema, kidume atakaye
jitokeza akaweza kunipa ujauzito nitamjengea nyumba ya kisasa…
…Nyumba ya vyumba vitatu. Kimoja selfu. Sebule kubwa, toilet ya jumuiya,
stoo, bafu na choo ikiwa imezungukwa na ukuta wa ulinzi," alisema Wolper
Aidha Wolper alisema kuwa anasubiri wakati wa Mwenyezi Mungu maana yeye
ndio anayetoa baraka hiyo.