Picha Kwa Hisani
Mwigizaji nguli kutoka Bara la Asia, Jackie Chan amefunguka kuwa atatoa sehemu ya utajiri wake unaofikia Dola za Marekani 370 milioni (takriban Shilingi bilioni 39) kwa watu wenye uhitaji kuliko kumpa mwanawe wa kiume kwa jina Jaycee.
Muigizaji huyo mwenye umri wa miaka 67, alitoa maelezo kuwa ameamua kutompa urithi huo wa utajiri Jaycee mwenye umri wa miaka 39 kwa kigezo kuwa kama mwanae ana uwezo wa kujitafutia pesa zake mwenyewe.
Jaycee ni mtoto pekee wa Chan na mkewe, Joan Lin waliooana mwaka 1982. Jay ni muigizaji na pia ni mwanamuziki. Mwaka 2014, aliwahi kukamatwa na dawa za kulevya na Chan alitumia nguvu kubwa kuomba radhi mbele ya umma kuhusiana na hilo.