Picha kwa hisani –
Shirika la utetezi wa haki za kibinadamu la MUHURI limeitaka mamlaka ya IPOA kuidhinisha uchunguzi kuhusu utendakazi wa maafisa wa polisi wa kituo cha Inuka eneo la Likoni.
Hii ni baada ya Mzee mmoja kwa jina la George Mburu kupigwa hadi akavunjwa mguu wake wa kulia alipokuwa amezuru kituo hicho ili kuripoti tukio la wizi.
Kulingana na Mburu, japo maafisa hao walimpeleka katika hospitali moja ya kibinafsi eneo hilo,kulingana na madaktari polisi hao walimuangusha Mburu mlangoni na kisha wakaondoka na kumwacha akivuja damu.
Afisa wa maswala ya dharura wa Shirika la MUHURI Francis Auma amesema tayari Shirika hilo limewasilisha lalama hizo kwa IPOA na linasubiri kauli ya Tume hiyo kabla ya kuchukua hatua za kisheria dhidi ya polisi waliohusika na dhuluma hiyo.