Huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya kimataifa ya haki za kibinadamu shirika lisilokuwa la kiserikali la Inform Action limeahidi kupigania haki ya jamii na kukabiliana kikamilifu na ukiukaji wa haki za kibinadamu.
Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Joseph Simeka amesema kuwa shirika lao litazidi kuhamasisha vijana kuhusiana na haki zao na vilevile kusukuma kukabiliwa kisheria kwa wanaokiuka haki za kibinadamu.
Simeka amesema kuwa wanajamii wengi hukandamizwa na kunyimwa hata haki ya kujieleza.
Mkurugenzi huyo amewataka wananchi kusimama na kupigania haki zao ili kukomesha ukiukaji wa haki unaoshuhudiwa nchini na kote ulimwenguni.
Taarifa na Mariam Gao.