Ni filamu ambayo imezua hamu na ghamu miongoni mwa wapenzi wa filamu humu nchini. Kila mtu anasubiria siku ambayo itazinduliwa rasmi. Jina lake ni Subira na ilitengenezwa kisiwani Lamu na Jijini Nairobi.
Ni filamu ambayo mwanzo iliundwa kama filamu fupi lakini sasa wakenya watakuwa na fursa ya kutazama filamu ndefu baada ya filamu hiyo kutengenezwa upya.
Ikiwa filamu fupi Subira ilishinda tuzo 15 za kimataifa.
Filamu hii inazungumzia uhuru wa mwanamke na ukandamizaji wake katika jamii.
Maudhui haya yanajitokeza kupitia muigizaji kwa jina “Subira”. Kulingana na mila na desturi hawezi kufanya mambo yanayofanywa na wanaume pekee kama vile kuogelea. Moyoni mwa subira hata hivyo mshawasha wa kuwa mpiga mbizi haumpi nafasi ya kufuatilia mila na desturi.
Tizama filamu fupi hapa.