Story by Our Correspondents-
Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC imepongeza hatua ya Wizara ya Elimu nchini ya kutangaza mapema kufungwa kwa shule hasa za msingi ili kupeana nafasi ya zoezi la uchaguzi mkuu.
Naibu Mwenyekiti wa Tume hiyo Juliana Cherera amesema mara nyingi maeneo ya shule yamekuwa wakitumika kama vituo vya kupigia kura na itakuwa vyema iwapo tume hiyo itapewa nafasi ya kuandaa vituo hivyo na mapema.
Juliana amesisitiza umuhimu wa vituo hivyo kutumika vyema na wapiga kura ili baadaye wanafunzi waendelee na masomo kulingana nna ratiba ya masomo huku akiwaonya wapiga kura dhidi ya kuharibu maeneo hayo.
Wakati uo huo amewarai wakenya kujitokeza kwa wingi wakati wa uchaguzi mkuu na kushiriki zoezi la upigaji kura kwa kuzingatia amani.