Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC imetangaza kwamba wapiga kura milioni 22,120,458 wamesajiliwa kushiriki upigaji kura katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9.
Mwenyekiti wa tume ya IEBC Wafula Chebukati ametoa tangazo hilo baada ya kukamilika kwa zoezi la kukagua sajili ya wapiga kura,zoezi liliendelezwa na kampuni ya KPMG.
Chebukati aidha ameeleza kwamba kati ya wapiga kura hao zaidi ya milioni 22 ,idadi ya wanawake ni ndogo wakiwa na asilimia 49.12 huku wanaume wakiwa ni asilimia 50.88,na kwamba wapiga kura elfu 246,265 waliofariki wametolewa katika sajili ya wapiga kura huku wapiga kura walioko nje ya nchi wakiwa ni asilimia 0.05.
Akizungumza na wanahabari hii leo Chebukati aidha amesema ni jumla ya vituo vya kupigia kura 46,232 vilivyoidhinishwa kote nchini vitakavyotumika wakati wa uchaguzi.