Story by Our Correspondents –
Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC imeweka wazi kwamba haina uwezo wa kuwazuia wanasiasa kutofanya kampeni za mapema bali watawahimiza kuhakikisha wanadumisha amani wakati wa kampeni zao.
Mwenyekiti wa Tume hiyo Wafula Chebukati amesema Tume hiyo haina mamlaka ya kufanya hivyo bali wanasiasa wenyewe wanafaa kuzingatia amani na wala sio kuvuruga usalama wa taifa hili.
Katika kikao na viongozi wa baraza la makanisa nchini NCCK, Chebukati amewahimiza viongozi hao wa kidini kuwashauri wanasiasa kutambua umuhimu wa taifa lenye amani ili kuwepo na uchaguzi wa amani.
Wakati uo huo amewataka vijana kujitokeza kwa wingi wakati wa zoezi la usajili wapiga kura mwaka ujao ili waweze kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu ujao.