Story by Our Corresponents-
Mgombea wa kiti cha urais kupitia tiketi ya chama cha Safina Jimmy Wanjigi amekosa kuidhinishwa na tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kuwania kiti hicho wakati wa uchaguzi mkuu wa Agosti 9.
Mwenyekiti wa Tume ya IEBC Wafula Chebukati amesema Tume hiyo haiwezi kumuidhinisha Wanjigi kuwa mgombea wa kiti hicho, ikimtaka kuwasilisha stakabadhi zake halali za shahada ya degree.
Chebukati amesema tume hiyo inazingatia usawa na uwazi pamoja na saini halali za kuonyesha wazi kwamba wananchi wameridhia na uteuzi wake kama mgombea wa urais.
Akizungumza baada ya kukosa kuidhinishwa na tume hiyo, Mgombea huyo wa rais kupitia tiketi ya Safina Jimmy Wanjigi amesema atafanya kila juhudi kuhakikisha majina yake yanawekwa katika sajili ya wagombea wa urais huku akisema ni lazima sheria azingatiwe.