Picha kwa hisani –
Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC imeidhinisha nakala maalum zitakazotumika wakati wa kukusanya saini milioni moja za wakenya za kuidhinishwa ripoti ya BBI.
Mwenyekiti wa tume hio Wafula Chebukati amesema ili kuthibitisha wapiga kura ni lazima watakaotia saini wajaze maelezo muhimu kuwahusu kwenye nakala hizo ikiwemo majina yao, vituo vya kupigia kura, miongoni mwa maelezo mengine.
Chebulati amesema maelezo hayo ikiwemo nambari za vitambulisho na maeneo bunge ya wanaotia saini,yatawezesha tume ya IEBC kudhibitisha maelezo kuhusu wanaounga mkono ripoti hio.
Haya yanajiri huku Rais Uhuru Kenyatta na mwenzake kinara wa ODM Raila Odinga wakitarajiwa kuzindua rasmi zoezi hilo la kukukusanya saini za ripoti ya BBI hapo kesho katika jumba la mikutano la KICC jijini Nairobi.