Story by Ephie Harusi-
Meneja wa uchaguzi katika kaunti ya Kilifi Abdulwahid Hussein amesema huenda zoezi la usajili wa wapiga kura likatatizwa katika kaunti hiyo kutokana na kushuhudiwa kwa baa la njaa.
Akizungumza mjini Kilifi, Hussein amesema kuna zaidi ya wadi 16 katika kaunti ya Kilifi ambazo zinahitaji msaada wa dharura wa chakula na anahofia kwamba huenda wakaazi wakakosa kujitokeza kusajiliwa kama wapiga kura.
Hussein amewahimiza wakaazi kujitokeza na kujisajili kama wapiga kura katika vituo mbalimbali vya kujisajili licha ya kupitia changamoto mbalimbali.
Kwa upande wake Afisa wa mipango katika shirika la kijamii la KECOSCE Kibwana Hassan amesisitiza haja ya wakaazi kujitokeza kwa wingi ili wajiandikishe kama wapiga kura.