Picha kwa hisani –
Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC imeahidi kujiandaa vyema katika uchaguzi mdogo wa Msambweni, Wadi ya Wundanyi/Mbale na Dabaso kule kaunti ya Kilifi.
Afisa wa IEBC anayesimamia uchaguzi wa ubunge wa Msambweni Yusuf Abubakar Mohammed amesema tayari vifaa vya uchaguzi huo vimesambazwa katika vituo vyote vya kupigia kura tayari wa uchaguzi huo.
Akizungumza na Wanahabari baada ya kukamilisha matayarisho ya uchaguzi huo, Yusuf amesema swala la kujikinga na maambukizi ya Corona limepewa kipau mbele katika uchaguzi huo huku akipinga madai ya Tume hiyo kuegemea wa wanasiasa.
Kulingana na Tume ya IEBC, sajili ya wapiga kura katika eneo bunge hilo ni 69,003 ambao wanatarajiwa kushiriki uchaguzi huo na vituo vya kupigia kura vikiwa 129 huku wagombea wa uchaguzi huo wakiwa wanane.