Story by Our Correspondents-
Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC imeungana na viongozi wa kidini wa baraza la kitaifa la makanisa NCCK na Muungano wa Maaskofu wa Kanisa Katoliki na kufanya maombi maalum ya uchaguzi mkuu.
Akizungumza wakati wa maombi hayo ya amani yalioandaliwa jijini Nairobi, Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati wamewaomba viongozi wa kidini kuliombea taifa hili sawa na maafisa wa IEBC ili kufanikisha uchaguzi huru na haki.
Chebukati ameweka wazi kwamba wagombea waliosajiliwa kushiriki uchaguzi ni elfu 16 na wanalenga kuwania viti 1,882 na watakaotangazwa ni watu elfu 14 pekee huku akiwataka wale watakaoshindwa katika uchaguzi huo kukubali matokeo.
Kwa upande wao viongozi wa kidini wamesisitiza haja ya wakenya kutambua mafunzo ya mwenzi Mungu na kushiriki uchaguzi wa amani huku wakiahidi kuendelea kuwashauri wananchi kudumisha amani.