Picha kwa Hisani –
Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC ikiongozwa na mwenyekiti wake Wafula Chebukati imezindua rasmi zoezi la kukagua saini milioni nne zilizokusanywa ili kuidhinisha ripoti ya BBI.
Akizungumza wakati wa kuzindua zoezi hilo katika ukumbi wa BOMAS jijini Nairobi,Chebukati amesema kati ya watu waliotuma maombi kufanya kazi hio ni watu 400 pekee waliopewa nafasi hio baada ya kufanyiwa ukaguzi unaostahili.
Chebukati amewataka maafisa hao kuendeleza zoezi hilo la kukagua saini za BBI kwa kuzingatia sheria za tume hio ya IEBC ikizingatiwa kwamba tayari wamekula kiapo ili kuendeleza zoezi hilo.
Chebukati aidha amewataka maafisa hao waliopewa jukumu la kukagua siani za ripoti za BBI kuendeleza kazi hio kwa kuzingatia sheria za kuzia maambukizi ya virusi vya corona.
Itakumbukwa kwamba mnamo tarehe 10 mwezi huu wa disemba,jopo la BBI liliwasilisha saini 4.4 kwa tume ya IEBC,ambapo BBI inaitaji saini milioni 1 kabla ya kuidhinishwa na kuwasilisha katika mabunge ya kaunti kujadiliwa.