Picha kwa hisani –
Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC imewaidhishwa zaidi ya wagombea 8 wanaowania kiti cha ubunge wa Msambweni katika uchaguzi mdogo ulioratibiwa kufanyika mwezi Disemba 15 mwaka huu.
Sheikh Abdulrahman Mahmoud, Mgombea wa kiti hicho kupitia chama WIPER ameidhishwa rasmi na Tume hiyo baada ya mgombea wa kiti hicho kupitia chama cha ODM Omar Iddi Boga kuidhinishwa mapema leo asubuhi.
Abdulrahma aliyeandamana na Mwenyekiti wa kitaifa chama cha Wiper Balozi Chirau Ali Mwakwere, Mbunge wa Embakasi South Julius Mawathe pamoja na Millicent Odhiambo Katibu mkuu wa Chama cha Wiper, amesema yuko tayari kwa kinyang’anyiro hicho.
Uchaguzi huo hata hivyo umewavutia wagombea 11, huku wanne kati yao wakiwa wagombea huru na wengine kutoka vyamba mbalimbali vya kisiasa nchini.