Story by Our Correspondents –
Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC imekosoa kauli zilizotolewa na Mbunge wa Gatundu kusini Moses Kuria kwamba tume hiyo haina mamlaka ya kusikiza kesi dhidi yake.
Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati amesema kauli zilizotolewa na Moses Kuria ni kejeli kwa tume hiyo na ni lazima kiongozi huyo afike mbele ya tume hiyo na kuhojiwa bila ya kukosa.
Chebukati amesema kesi hiyo itaendelea na ni lazima Mbunge huyo wa Gatundu kusini kufika mbele ya tume hiyo mnamo tarehe 7 mwezi Aprili mwaka huu ambapo kesi dhidi yake itasikizwa.
Moses Kuria ambaye alifika mbele ya tume hiyo mapema leo akiwa ameandamana na mawili wake Ndegwa Wahome na Geofrey Omenke, anadaiwa kutoa matamshi ya kukanganya kwamba akiwa pamoja na wanzake waliisaidia serikali ya Jubilee kuiba kura wakati wa uchaguzi uliopita.
Hata hivyo Makamishna wa IEBC wamedai kwamba matamshi ya Kuria yametia dosari uhalali wa matokeo ya urais ya mwaka wa 2017, wakisema kauli kama hizo huenda zikachangia mgawanyiko wa kisiasa nchini.