Story by Mimuh Mohamed –
Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC imetangaza kumchagua aliyekuwa seneta wa Samburu Sammy Leshore kuchukua nafasi ya Isaac Mwaura kama seneta maalum.
Tume ya IEBC chini ya Mwenyekiti wake Wafula Chebukati imechapisha tangazo hilo katika gazeti rasmi la serikali kwamba Leshore atakuwa mwakilishi wa walemavu katika bunge la seneti.
Hatua ya IEBC imejiri masaa kadhaa baada ya Mahakama kuu kutoa agizo la kuzuia Isaac Mwaura kupokonywa nafasi hiyo huku Mwaura akikata rufaa dhidi ya hatua hiyo ya IEBC.
Mvutano huu umejiri baada ya spika wa bunge la seneti Ken Lusaka siku ya Jumanne juma hili kupitia gazeti rasmi la serikali alitangaza kuwa wazi nafasi hiyo ya Isaac Mwaura.