Story by Salim Mwakazi –
Idara ya Mahakama imelaumiwa kwa kushindwa kuzishughulikia kesi za dhulma za kijinsia zinazowasilishwa Mahakamani.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la kijamii la Sauti ya wanawake Millicent Odhiambo amesema hali hiyo imechangia waathiriwa wa dhulma hizo kuhisi kunyanyasika kwa kukosa haki.
Akizungumza na Wanahabari, Millicent amesema kucheleweshwa kwa kesi hizo kusikizwa na kuamuliwa Mahakamani kumechangia wakenya wengi kutokuwa na imani na utendakazi wa idara ya Mahakama.
Kwa upande wake Kadhi wa Mahakama ya Kwale Sheikh Salim Mwaito amesema idara ya Mahakama inajitahidi kuhakikisha kila mtu anapata haki kwani kesi zinazowasilishwa Mahakamani husikizwa kwa wakati.