Picha kwa hisani –
Idara ya usalama katika Kaunti ya Mombasa imezindua upya oparesheni dhidi ya magenge ya kihalifu katika Kaunti hiyo.
Kamishna wa Kaunti ya Mombasa Gilbert Kitiyo amesema japo hali ya usalama imeimarika katika Kaunti hiyo, huenda magenge hayo yakatumia msimu wa sherehe za mwisho wa mwaka kuwahangaisha wakaazi.
Akizungumza baada ya kukutana na wadau wa usalama Kaunti hiyo, Kitiyo amesema ni wajibu wa wazazi na jamii ya Kaunti hiyo kuwashauri vijana kuyaasi magenge ya kihalifu la sivyo yaangamizwe.
Kitiyo aidha amesema taifa na hasa kaunti ya Mombasa bado iko katika hatari ya kushuhudia maambukizi ya virusi vya Corona na ni sharti kila mkaazi na wageni wanaozuru Kaunti hiyo kujivinjari msimu huu wa sherehe kuchukua tahadhari.