Picha kwa hisani –
Idara ya usalama kaunti ya Kwale inashirikiana na wavuvi kutoka maeneo bunge ya Kinango na Lunga-lunga kuwanasa raia wa kigeni wanaingia humu nchini bila vibali kupitia bahari hindi.
Afisa mkuu wa polisi katika eneo bunge la Lunga – lunga Peter Nzimbi amesema idadi kubwa ya raia wa kigeni wanaoingia nchini bila vibali hutumia njia za mkato kupitia bahari hindi katika maeneo hayo.
Nzimbi amesema tayari wamefanikiwa kuwanasa raia wa kigeni walioingia nchini bila vibali baadhi wakiwa raia wa taifa la Tanzania na ambao kwa sasa wanazuiliwa na maafisa wa polisi.
Hata hivyo Nzimbi ameendelea kuwaonya raia wote wanaohusika na kuwahifadhi raia hao wa kigeni kwamba watachukuliwa hatua kali za kisheria.