Shirika la kutetea haki za kibinadamu la Haki Africa limeitaka idara ya usalama nchini kuweka ulinzi wa kutosha kwa watalii wa kigeni wanaozuru humu nchini na hususan eneo la pwani.
Akizungumza jijini Mombasa, mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Hussein Khalid amesema visa vya watalii wa kigeni kuhangaishwa na kutekwa nyara vimekithiri kanda ya pwani, akisema hatua hiyo ni ukiukaji wa haki za kibinadamu.
Khalid amesema iwapo jitihada mwafaka hazitaidhinishwa ili kuvikabili visa aina hii, huenda sekta ya utalii kanda ya Pwani ikaathirika pakubwa.
Kauli yake imejiri baada ya mtalii moja raia wa Italai kutekwa nyara na watu wasiojulikana usiku wa kuamikia siku ya Jumanne eneo la Chakama kaunti ya Kilifi.
Taarifa na Hussein Mdune.