Idara ya usalama kaunti ya Kwale imewataka wakaazi wa kaunti hiyo kushirikiana nayo ili kukabiliana na uhalifu.
Akiongea na mwanahabari wetu kamishna wa kaunti ya Kwale Karuku Ngumo amefichua kuwa idara hiyo imezindua nambari maalum ya mawasiliano kati yake na wakaazi.
Ngumo ametaja kuwa nambari hiyo ambayo ni 22, 068 itatumika na wakaazi kutuma ujumbe wanaposhuhudia ama kupata tetesi zozote kuhusiana na matukio ya kihalifu.
Wakaazi wanaotuma ujumbe watahitajika kuandika jina la kaunti ili ujumbe huo ufikie kamishna wa kaunti.
Afisa huyo tawala amesema kuwa mbali na kumulika uhalifu nambari hiyo itasaidia afisi ya kamishna kutambua utendakazi wa maafisa wa usalama.
Taarifa na Mariam Gao.