Picha kwa Hisani –
Idara ya usalama imewataka wavuvi katika kaunti ya Lamu kujitokeza na kusajiliwa ili wapate vitambulisho maalum vitakavyowawezesha kutambuliwa na maafisa wa polisi wanaoendeleza oparesheni za kiusalama baharini.
Akihutubia wakaazi kamishna kaunti ya Lamu Irungu Macharia amesema zoezi la kukabidhi vitambulisho wavuvi hao linalenga kusaidia polisi kuwatambua magaidi kutoka taifa la Somalia wanaoingia kaunti ya Lamu kupitia bahari hindi.
Hata hivyo wavuvi katika kaunti hio wamelalamikia kuhangaishwa mara kwa mara na maafisa wa usalama wakisema huenda wakapitia mahangaiko hayo hata watakapopewa vitambulisho hivyo.
Haya yanajiri siku chache baada ya wavuvi wa kike katika kaunti ya Lamu kutaka kukabidhiwa vitambulisho ili wawe salama wanapoendeleza uvuvi baharini.