Viongozi katika kaunti ya Kilifi sasa wanazitaka idara zinazohusiska na maswala ya ujenzi wa nyumba, kuanzisha uchunguzi kuhusiana na mkasa wa kuporomoka kwa jumba moja mjini Malindi, uliosababisha kifo cha mtu moja na kujeruhiwa kwa watu 23.
Wakiongozwa na gavana wa kaunti ya Kilifi Amason Jeffa Kingi viongozi hao wamesema kuwa kuporomoka kwa jumba hilo kumesababisha hasara ya mali yenye thamani kubwa.
Mbunge wa Kilifi–Kazkazini Owen Baya ameitaka halmashauri ya ujenzi nchini kuanzisha uchunguzi na kuyavunja majumba yanayojengwa kinyume cha sheria mjini Malindi.