Idara ya mahakama nchini imehimizwa kuwa katika mstari wa mbele kupigania haki ili kusitisha dhuluma na mahangaiko miongoni mwa wakaazi hapa Pwani.
Afisa wa maswala ya dharura haki na sheria katika shirika la kutetea haki za kibinadamu nchini la MUHURI Fahad Changi amesema kwamba idara ya mahakama ina mchango mkubwa katika harakati za utetezi wa haki za kibinadamu.
Changi amesema kwamba kucheleweshwa kwa kesi kumepelekea mahangaiko na kukata tamaa miongoni mwa wapwani akisema iwapo idara ya mahakama itachukua muda mfupi kusikiza kesi mbalimbali na kuzisuluhisha, Wapwani wengi watapata haki.
Taarifa Na Gabriel Mwaganjoni