Story by Gabriel Mwaganjoni –
Shirika la utetezi wa haki za kibinadamu la ‘Sisters For Justice’ limeitaka idara ya upelelezi nchini DCI kuidhinisha uchunguzi wa dharura kuhusiana na visa vya watu kutekwa nyara na kuuwawa kinyama.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo Nailla Abdallah amesema matukio hayo ya kutisha yanapaswa kuchunguzwa na kudhibitiwa kwani yamewatia hofu wananchi mashinani.
Akizungumza katika eneo la Kisauni kaunti ya Mombasa, Nailla amesema misururu ya visa vya utekaji nyara na mauaji ya kiholela yameonekana kushamiri mno katika miji ya Nairobi na Mombasa.
Mwanaharakati huyo wa kijamii amesisitiza umuhimu wa idara ya upelelezi nchini kufanya kila juhudi ili kuwakabili wahusika wakuu wa unyama huo.