Story by Ngombo Jeff-
Idara ya afya katika kaunti ya Kilifi imesema takriban watoto 100 wanaugua ugonjwa wa kisukari katika mji wa Malindi.
Kulingana na mtaalam wa ugonjwa wa kisukari katika hospitali ya Malindi Nuru Kibirige, idadi hiyo ni kati ya wale waliofanyiwa vipimo huku wengine zaidi wakihofiwa kuugua maradhi hayo.
Kibirige amesisItiza haja ya wazazi wanaougua ugonjwa wa kisukari kuhakikisha familia zao zinafanyiwa vipimo vya ugonjwa huo ili kuwawezesha kupata matibabu ya uongojwa huo.
Hata hivyo mtaalam huyo wa afya amesema idara ya afya, tayari imebuni kitengo maalum ikishirikiana na wadau wengine wa sekta ya afya ili kukabiliana na makali ya ugonjwa huo.