Hamasa ambazo zimekuwa zikitolewa na Serikali ya Kaunti ya Mombasa na Wauguzi wa nyanjani kwa kiwango kikubwa zimepelekea Wakaazi wengi wa Kaunti hiyo kuzuru vituo vya afya ili kujua hali zao za virusi.
Muuguzi wa Shirika la wauguzi la Al-shifaa Welfare Group Bi Fatuma Omar Mohammed amesema kwamba ikilinganishwa na hapo awali ambapo Wakaazi wengi walikuwa wakihofia kuzuru vituo vya afya ili kujua hali zao, kwa sasa Wakaazi wengi wanazuru vituo hivyo ili kupewa ushauri.
Akizungumza Mjini Mombasa, Bi Omar amesema kwamba Shirika hilo la wauguzi wa umma limeimarisha mikakati yake likishirikiana na wadau mbalimbali wa afya kwa lengo la kuiwezesha jamii sio tu katika Kaunti ya Mombasa bali kote Pwani kupata elimu ya kutosha kuhusu swala la virusi vinavyochangia ukimwi,
Amesisitzia umuhimu wa jamii kamwe kutohofia kujua hali zao za virusi kwani kutambua hali zao kutazuia maambukizi zaidi na kuwawezesha wale waliyoambukizwa kuishi maisha ya kawaida na kutekeleza majukumu yao kikamilifu katika jamii.
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.