Story by Our Correspondents–
Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC inaendeleza zoezi la upigaji kura katika vituo mbalimbali vya kupigia kura kote nchini.
Maafisa wa IEBC wakiongozwa na Mwenyekiti wao Wafula Chebukati wameanza rasmi zoezi hilo mwendo wa saa kumi na mbili asubuhi.
Idadi kubwa ya wakenya wamejitokeza na kushiriki uchaguzi huo wa amani huku baadhi ya wananchi wakilalamikia kushuhudiwa kwa fulani ndefu katika vituo nbalimbali vya upigajia kura.
Hata hivyo maafisa wa usalama wameonekana kushika doria kikamilifu ili kuhakikisha uchaguzi huo unashuhudia amani.