Story by Mwanaamina Fakii –
Idara ya Afya kaunti ya Kwale imesema idadi kubwa ya wakaazi katika eneo bunge la Matuga wamejitokeza na kuchukua vyandarua vya kuzuia Mbu.
Afisa wa afya ya jamii katika eneo hilo Anne Kache amesema zoezi la ugavi wa vyandarua hivyo lilianza vyema na litaendelea hadi siku ya Jumapili ili kuhakikisha kila mkaazi aliyesajiliwa anapata vyandarua hivyo.
Kache amewahimiza wakaazi waliopata vyandarua hivyo kuhakikisha wanavianika kwa masaa 24 kabla ya kuanza kuvitumia huku akisema changamoto zilizoshuhudiwa wakati wa ugavi wa vyandarua hivyo zimetatuliwa.
Wakati uo huo amewahimiza wakaazi kuhakikisha wanatumia vyandarua hivyo kwa kuzingatia masharti ya Wizara ya Afya nchini ili kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa Malaria.