Utafiti uliofanywa na shirika la Moving the Goal Post (MTG) umebaini kuwa asilimia kubwa ya vijana waliofikisha umri wa kubalehe katika gatuzi dogo la Matuga kaunti ya Kwale hawana elimu ya kutosha kuhusu afya ya uzazi.
Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Dorcas Amakombe amefichua kuwa ukosefu wa maafisa wa afya katika hospitali na zahanati kuwapa vijana elimu kuhusu afya ya uzazi imechangia wengi wao kutokuwa na elimu hiyo.
Amakombe ametaja kuwa shirika hilo kupitia wadau mbalimbali litaihimiza serikali ya kaunti ya Kwale kutenga fedha za kutosha kuendeleza elimu hiyo ili kuhakikisha vijana wanapata elimu ya kutosha kuhusu afya ya uzazi.
Utafiti huo ulifanywa katika gatuzi dogo la Matuga wadi za Tsimba- Golini,Waa na Tiwi huku shirika hilo likiahidi kuendeleza utafiti huo maeneo mengine ya Kaunti ya Kwale.
Taarifa na Mariam Gao.