Picha kwa hisani –
Ibada ya wafu ya aliyekua waziri mwendazake Simeon Nyachae imeandaliwa hii leo katika kanisa la kisabato la Maxwel jijini Nairobi.
Viongozi mbali mbali wamehudhuria ibada hio akiwemo aliyekua waziri mkuu Raila Odinga,Musalia Mudavadi wa ANC ,Waziri wa usalama wa ndani dkt Fred Matiangi, na viongozi wengine.
Akiwahutubia waombolezaji wakati wa Ibada hio Kinara wa ANC Musalia Mudavadi amesema amejifunza masuala mengi ya kisiasa kutoka kwa mwendazake Nyachae na ambayo yamemjenga kiuongozi.
Kinara wa WIPER Kalonzo Musyoka pia amehutubia katika hafla hio.
Ibada ya mazishi ya mwendazake Nyachae inatarajiwa kufanyika katika uwanja wa Nyaturago katika kaunti ya Kisii na marehemu Nyachae ambae aliaga dunia tarehe moja mwezi huu wa February akiwa na miaka 88, atazikwa siku ya jumatatu juma lijalo katika eneo la Nyosia kaunti ya Kisii.