Picha kwa hisani –
Ibada ya ukumbusho wa aliyekua rais wa pili wa taifa hili mwendazake Daniel Toroitich Arap Moi imefanyika huko Kabarak ikiwa ni hii leo ni mwaka mmoja tangu alipoaga dunia mnamo tarehe nne mwezi februari mwaka uliopita.
Ibada hio imehudhuriwa na watu wachache pekee ikiwemo familia ya mwendazake Moi pamoja na marafiki wa karibu wa familia hio akiwemo Rais Uhuru Kenyatta na kinara wa ODM Raila Odinga.
Baadhi ya viongozi waliohudhuria ibada hio wamesema mwendazake Moi ataendelea kukumbukwa kwa miradi ya elimu na miradi mengine ya maendeleo aliyoyaidhinisha katika maeneo mbali mbali ya taifa wakati wa utawala wake.
Viongozi waliohudhuria hafla hio ikiwemo kiongozi wa taifa Uhuru Kenyatta wanaendelea kutoa hotuba zao.
Mwendazake Moi alihudumu kama rais wa taifa hili kwa miaka 24 kabla ya kuachia madaraka mwaka 2002,na pia alihudumu kama makamo wa rais nchini kwa miaka 11 na aliaga dunia akiwa na miaka 95.