Picha kwa Hisani –
Mahakama inatarajiwa kutoa hukumu dhidi ya washukiwa watatu wa shambulizi la kigaidi katika jumba la kibiashara la westgate Nairobi,lililotekelezwa mwaka 2013 na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 67.
Hakimu Francis Andayi anaendelea kusoma uamuzi wa kesi hio ambapo watuhumiwa hao akiwemo Mohammed Ahmed, Liban Abdullahi and Hussein Mustafa wametuhumiwa kwa kutoa usaidizi kwa kundi la kigaidi la alshabaab kutekeleza shambulizi hilo.
Akisoma nakala za ushahidi hakimu Andayi amesema washukiwa hao wameshtakiwa kwa makosa 12 ikiwemo kupatikana na kanda za video zinazowapa mafunzo ya kutekeleza ugaidi.
Vikao vya kesi hio bado vinaendeleo na uamuzi itatolewa muda wowote kuanzia sasa,kesi hio inaendeleo huku maafisa wa kupambana na ugaidi ATPU wakiwa wameimarisha ulinzi katika eneo hilo.