Story by Our Correspondents-
Mgombea wa kiti cha ubunge wa Matuga kwa tiketi ya chama cha Jubilee Hassan Chidzuga Fundi amepinga madai yanayoenezwa na wapinzani wake wa kisiasa kwamba yeye ni mradi wa baadhi ya wanasiasa.
Katika mahojiano ya kipekee na kituo cha Radio Kaya kwenye kipindi cha Voroni Enehu, Hassan amesema alitawazwa na wazee wa eneo bunge hilo ili kuwania kiti hicho kutokana na juhudi zake za kupigania haki za wakaazi wa Matuga.
Hassan amesema ana malengo bora ya kuhakikisha wakaazi wa Matuga wananufaika kimaendeleo huku akidai kwamba chama cha Jubilee kiko imara katika kuhakikisha wananchi wananufaika.
Wakati uo huo ameahidi kuhakikisha anawajenga uwezo vijana kupitia vipaji vyao, akidai kwamba hatua hiyo itahakikisha vijana wanajitegemea wenyewe huku akidai kwamba mgoa wa sekta ya utalii katika eneo hilo utawanufaisha wakaazi.