Picha kwa hisani –
Katibu mkuu wa muungano wa matabibu nchini George Gibore amesema huenda baraza la magavana linauhasama na wizara ya afya nchini ndiposa likajitenga na mkataba wa makubaliano uliotiwa saini wa kuwezesha matabibu kusitisha mgomo.
Akizungumza na wanahabari Gibore amesema wameshangazwa na hatua ya baraza hilo kujitenga ghafla na mkataba huo licha ya viongozi wakuu wa baraza hilo kuhusishwa katika hatua zote za mazungumzo za kutengeneza makataba huo.
Gibore amesema amesema matabibu watarejea tena kwenye mgomo iwapo baraza la magavana na wizara ya afya hawataafikiana kuhusu jinsi ya kutekeleza matakwa yao iwapo makataa ya saa 48 waliotoa yatakamilika.
Matabibu walisitisha mgomo wao siku ya ijumaa juma lililopita mgomo uliodumu kwa siku 26,baada ya kutia saini mkataba wa kurejea kazini na wizara ya afy,ile ya leba na baraza la magavana,mkataba ambao sasa baraza la magavana limeukana kwa madai ya kutohusishwa kwenye mazungumzo.