Picha Kwa Hisani – WGT Empire Instagram Page.
Kimya kingi kina mshindo mkuu! Baada ya kupotea kwenye tasnia ya burudani kwa Zaidi ya mwaka mmoja, mwanamuziki kutoka Malindi Mnyamwezi arudi Kwa kishindo na wimbo wake mpya kwa jina Huba.
Msanii huyo ambaye yupo chini ya usimamizi wa labo ya Waghetto Empire, anazidi kutamba kwa ngoma hiyo aliyoizindua siku ya Jumatatu. Hii ni baada ya ‘Huba’ kupokelea vyema na mashabiki na wasanii wengi kumpa shavu kupitia mitandao ya kijamii.
Tofauti na kawaida yake, mwanamuziki huyu ambaye alitamba na ngoma yake Unavyonipa na hivi karibuni Kiroboto alikaa kimya kwa Zaidi ya mwaka huku mashabiki wake wakizua kila aina ya tetesi mitandaoni kuhusu kupotea kwake.
Ngoma hiyo imetengenezwa na mzalishaji muziki Bang Belly.
Unaizungumziaje ngoma hii mpya kutoka kwa Mnyamwezi?