Asilimia 70 ya hoteli katika eneo la Pwani zitalazimika kufunga shughuli zake za kibiashara kuanzia juma hili kutokana na makali ya virusi vya Corona yaliyopelekea hoteli hizo kukosa wageni.
Kulingana na mkurugenzi mkuu wa Chama cha wamiliki na wahudumu wa mahoteli Kanda ya Pwani Sam Ikwaye, hoteli hizo zilikuwa na matarajio makubwa ya kupata wageni hasa msimu wa Pasaka japo wimbi la tatu la Corona likasambaratisha matarajio hayo.
Ikwaye amesema wageni wengi waliyokuwa wameahirisha safari zao kuja humu nchini mwaka uliyopita walikuwa na matumaini makubwa ya kuzuru eneo hili msimu huo wa pasaka japo hali ikabadilika na kuathiri pakubwa sekta ya utalii nchini.